Thursday, March 17, 2016

SALAD YA CABBAGE, CARROT NA TANGO



INGREDIENTS

Cabbage  1/2
Carrot  2
Tango 1


NAMNA YA KUTAYARISHA


1. Kata cabbage nyembamba sana.
2. Zikwangue carrot zitoke nyembamba.
3. Kata tango vipande vidogo vidogo.
4. Kisha changanya pamoja tia kwenye bakuli.
5. Changa vizuri mchanganyiko wako vizuri..
6. Tia chumvi, ndimu alaf changanya vzuri..
    salad tayari kwa kuliwa na kitu chochote

PILAU YA KUKU


ingridients


Mchele wa basmati/wa kawaida 3vikombe
Kuku 1/2
Viazi 4vitunguu maji 2Kkitunguu saumu(garlic) iliyosagwa
Binzari nyembamba kijiko kimoja
Pilipili manga 1/2 kijiko cha chai
Karafuu nzima 8
Iliki nzima 6
Mdalasini nzima 5 vijiti 
Pilipili mbichi iliyosagwa kijiko kimoja cha chai
Chumvi 1/2 kidogo cha chai
Mafuta ya kupikia 1/4 kikombe














NAMNA YA KUANDAA

1. Osha mchele na loweka kwa muda, kutegemea na aina ya mchele.
2. Kata kuku vipande upendavyo, safisha kisha mchemshe kwa chumvi, pilipili iliyosagwa na      tangawizi.
3. Akiiva kuku, mtoe weka kando, bakisha supu katika sufuria.
4. Katika sufuria kaanga vitunguu hadi vigeuke rangi ya hudhurungi.
5.Tia tangawizi na binzari zote kaanga kidogo.
6. kisha tia viazi kaanga kidogo kisha tia tia vipande vyako vya kuku na supu acha ichemke     kidogo         kisha tia maji ukisie kutokana na mchele unaotumia.
7. Mwisho tia mchele koroga uchanganye na vitu vyote acha ichemke kiasi kisha funika na       punguza       moto mpaka uive(huku ukigeuzageuza)
8. Ukishakuwa tayari pakua kwenye sahani tayari kwa kula na salad na pilipili.