PILAU YA KUKU
ingridients
Mchele wa basmati/wa kawaida 3vikombe
Kuku 1/2
Viazi 4vitunguu maji 2Kkitunguu saumu(garlic) iliyosagwa
Binzari nyembamba kijiko kimoja
Pilipili manga 1/2 kijiko cha chai
Karafuu nzima 8
Iliki nzima 6
Mdalasini nzima 5 vijiti
Pilipili mbichi iliyosagwa kijiko kimoja cha chai
Chumvi 1/2 kidogo cha chai
Mafuta ya kupikia 1/4 kikombe
NAMNA YA KUANDAA
1. Osha mchele na loweka kwa muda, kutegemea na aina ya mchele.
2. Kata kuku vipande upendavyo, safisha kisha mchemshe kwa chumvi, pilipili iliyosagwa na tangawizi.
3. Akiiva kuku, mtoe weka kando, bakisha supu katika sufuria.
4. Katika sufuria kaanga vitunguu hadi vigeuke rangi ya hudhurungi.
5.Tia tangawizi na binzari zote kaanga kidogo.
6. kisha tia viazi kaanga kidogo kisha tia tia vipande vyako vya kuku na supu acha ichemke kidogo kisha tia maji ukisie kutokana na mchele unaotumia.
7. Mwisho tia mchele koroga uchanganye na vitu vyote acha ichemke kiasi kisha funika na punguza moto mpaka uive(huku ukigeuzageuza)
8. Ukishakuwa tayari pakua kwenye sahani tayari kwa kula na salad na pilipili.
No comments:
Post a Comment